Karibu katika nakala hii ambayo utazijua faida za kutoa machozi katika mwili wa mwanadamu.
Tafiti zilizofanywa zinasema kuwa mtu anapomaliza kulia hujihisi ahueni, kuwa na amani, stress hupungua na pia huona amerelax tofauti na kabla ya kulia.
Majibu
ya watafiti wetu
Mtafiti Bergman
(Mtafiti wa machozi) Alinukuliwa
akisema ”Kuzuia machozi huongeza viwango
vya shida na pia huchangia magonjwa yatokanayo na matatizo ya shinikizo la damu
magonjwa ya moyo na vidonda vya peptic”.
Mtafiti William
Frey (Biochemist) Alithibitisha
kuwa machozi hupunguza baadhi ya sumu
katika mwili wa mwanadamu kutokana na kuwa na wingi wa madini ya manganese na
homoni za prolactin.
Kutoa
machozi ni nini?
Kutoa machozi ni njia ya asili ya kuongeza hisia za
moja kwa moja kutoka moyoni lakini pia machozi ni njia ya kuongea vitu vingi
kwa wakati mmoja
Aina
za machozi ya mwanadamu
1. Emotional
tears
a. Ni
machozi yanayotoka kwa kuguswa na hisia (Kuumizwa
moyo).
2. Basal
tears/Lubricant tears
a. Ni
machozi ambayo hufanya macho yetu kuwa na majimaji muda wote ambayo husaidia
macho kuona vizuri
3. Reflex
tears
a. Ni
machozi ambayo mara nyingi hutoka pale kitu kinachokuwasha kikiingia machoni mfano vitunguu, sabuni, chumvi nk.
Faida
za kutoa machozi
1. Ni
njia nzuri ya kupunguza stress
2. Huonyesha
uwazi
3. Ni
moja ya njia ya kuongea mambo mengi kwa wakati mmoja
4. Hupunguza
kemikali mwilini
Wataalamu na watafiti wa machozi na afya ya
mwanadamu wanasema ukiwa na hali zifuatazo tafuta sehemu ya peke yako kasha
ruhusu kilio ambacho kitaruhusu machozi yatakayotiririka yenyewe na si kwa
kulazimisha.
Pia unapotoa machozi husisha na hisia zako za ndani
ili kuleta tiba sahihi na baada ya hapo utajihisi ahueni
1. Stress
2. Maumivu
a. Ya
moyo
b. Ya
mwili
3. Umekasirika
sana
4. Umeumizwa
5. Kumbukizi
zinazosononesha
6. Kujihisi
kutoa machozi
Zingatio
1. Usimzuie
mtu anayetoa machozi maana ni moja ya tiba ya kutibu maumivu ya ndani
2. Inashauriwa
mara baada ya kumaliza kutoa machozi jimwagie maji maana maji husaidia
kurekebisha joto la mwili na utajihisi kuwa mchangamfu na mwenye furaha
Sasa unaweza ukawa unapata machapicho yetu katika
email yako kwa kubonyeza kitufe cha SUBSCRIBE
kilichopo juu upande wa kulia na kisha weka email yako. **HUDUMA HII NI BURE**
Imeandaliwa
na
mafahealth.blogspot.com
Chini
ya udhamini wa MaFaSystems
Maoni