Mara nyingi tumezoea kutumia tunda hili katika matumizi mbali mbali ya majumbani mwetu na hata kwa biashara pia
Lakini je, unajua ni kitu gani kipo ndani ya tunda
hilo lililobarikiwa wingi wa mali zinazohitajika na mwanadamu ndani yake?
Nakala hii imeandaliwa kwa ajili yako wewe msomaji
ili upate kujifunza mengi kuhusu tunda hili
1. Ubuyu
huweza kutumika kuzuia kutapika na kuharisha
2. Ubuyu
tumika pia katika ujenzi wa neva za mwili
3. Ubuyu
husaidia afya kwa wenye wagonjwa wenye presha ya kushuka ana figo
4. Utumiaji
wa juisi ya ubuyu ni moja ya njia ya asili ya kusafisha figo vizuri
5. Kwa
wenye matatizo ya macho ubuyu huongeza nuru katika macho (Juisi yake)
6. Ubuyu
hupunguza na kuondoa sumu katika mwili wa mwanadamu
7. Ubuyu
umejazwa na vitamin C nyingi kuliko machungwa hivyo huongeza kinga ya mwili
8. Ubuyu
una madini mengine kama B2,B3, Calcium, Magnesium, Potassium na madini ya chuma
ambayo yote hutumika katika ujenzi wa mwili na afya ya akili
9. Ubuyu
ni mzuri katika ujenzi wa mifupa imara
10. Unga
wa ubuyu unatajwa kuwa ni moja kati ya vyakula vyenye madini na vitamin nyingi
Zingatio
1. Hakikisha
umetumia ubuyu mweupe(Ubuyu mweupe) unaouzwa masokoni
2. Jitahidi
kunywa glass moja au mbili kwa siku badala ya kutumia vinywaji vyenye kemikali
Jinsi ya kuandaa juisi hii
Kwa unga wa ubuyu
1. Andaa
maji safi
2. Andaa
asali(Kama utapendelea)
3. Chukua
unga wa ubuyu weka katika chombo kisafi na kikavu
4. Ongeza
maji hakikisha juisi sio nzito sana
5. Weka
asali yako na unaweza ukanywa
1. Chemsha
maji kasha yachuje ili kuondoa uchafu
2. Weka
ubuyu wako kasha funika kwa muda hadi ulainike kasha koroga hadi zibaki mbegu
tu
3. Chuja
juisi yako na iko tayari kwa matumizi
Sasa unaweza ukawa unapata machapicho yetu katika email yako kwa kubonyeza kitufe cha SUBSCRIBE kilichopo juu upande wa kulia na kasha ukaweka email yako. **HUDUMA HII NI BURE**
Imeandaliwa
na
mafahealth.blogspot.com
Chini
ya udhamini wa MaFaSystems
Maoni