TAMBUA KAZI 31 ZA MAJI USIZOZIJUA

water

Tujiulize

Je, uliwahi kufikiria kwanini tunasema maji ni uhai?

Je, unafahamu kwanii wataalamu wa afya husisitiza unywaji wa maji kila siku?

Je, wajua kwamba baada ya hewa ya oksijeni maji ndio kitu kinachofuatia kwa kupewa kipaumbele katika mwili wa mwanadamu?


Zifuatazo ni kazi 31 usizozijua za maji katika mwili wa mwanadamu

1.      Katika maji tunapata oksijeni na hydrogen vitu ambavyo ni lulu ya mwili wetu

2.      Maji hutengeneza Ngozi kuwa nyororo na huzuia muonekano wa kuzeeka mapema

3.      Maji hutumika kama moja ya malighafu muhimu katika utengenezwaji wa seli

4.      Maji hupunguza uchovu na kuleta nguvu

5.      Mai huzuia kuzibika kwa mishipa ya ateri katika moyo

6.      Maji ni muhimu katika kurekebisha joto la mwili

7.      Maji hupunguza homa za asubuhi kwa mama mjamzito

8.      Maji huweza kutumika pia katika kuzuia ugonjwa wa mtoto wa jicho

9.      Maji huzuia shambulio la moyo na mshtuko

10.  Maji hukinga uharibifu wa vinasaba(DNA)

11.  Maji hupunguza maumivu ya ishara za kutokea kwa hedhi (Kwa wanawake)

12.  Maji huongeza ukuaji wa viinilishe muhimu katika chakula

13.  Maji husafisha mwili na kufanya njia ya mmeng’enyo wa chakula kubaki kuwa safi


14.  Maji huyeyusha dam una kuzuia isigande katika mzunguko wake

15.  Maji hupunguza mfadhaiko, pupa na kukata tamaa

16.  Maji ni wakala muhimu katika mmeng’enyo wa chakula (endapo yatatumiwa ipasavyo)

17.  Maji huweza kuongeza kinga na nguvu za mwili pia.

18.  Maji yakipungua mwilini husababisha seli kufa na kufanya mwili kukosa afya

19.  Maji hutumuka katika pia katika usafirishaji wa vitu mwilini

20.  Upungufu wa maji mwilini hupelekea kukosekana kwa hamu ya tendo la ndoa

21.  Maji hutumika katika kupunguza uzito na unene bila kufanya mazoezi

a.       Kupunguza kula na kuongeza kunywa maji mengi

22.  Maji hulainisha katika maeneo ya maungio na huzuia magonjwa ya yanisi na kupooza

23.  Maji huongeza nuru na mng’aro katika macho na kuhimili kuona vizuri

24.  Upungufu wa maji mwilini huhifadhi vijidudu nyemelezi ambavyo huleta magonjwa mwilini

25.  Maji huweza kubadili hali ya utegemezi wa vilevi kama pombe (Kama mtumiaji anahitaji kuacha haraka)

26.  Maji hutumika kuokoa na madhara ya kufunga choo na choo kigumu pia

27.  Maji husawazisha mfumo wa uzalishaji damu na kuzuia magonjwa kama anaemia

28.  Maji huepusha ndoto mbaya. (Unapoota ndoto mbaya mwili hujaribu kukuamsha. Kunywa glass 1 kisha lala tena)

29.  Maji ndio kichangamsho sahihi cha mwili wetu kisicho na madhara katika dunia hii

30.  Maji hutumika pia katika kusomba taka chafu mbalimbali hadi katika ini na figo kwa ajili ya kutolewa nje ya mwili

31.  Oksijen iliyopo katika maji husafiri haraka zaidi kuliko tunayoivuta kupitia mapafu

 

Kumbuka:


2.      Maji ndio kama fedha ya mwili. Kukosa maji mwilini ni saw ana kwenda dukani bila fedha

3.      Kunywa maji kidogo au hadi uhisi kiu si nzuri kiafya badala yake jenga mazoea ya kunywa maji kila siku.


Imehaririwa na 

Matayo F, Ayo

Maoni